Januari
9, 2023 Akiwa katika ukaguzi wa mapokezi ya wanafunzi hao upande wa Elimu
Sekondari Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda ameeleza kutoridhishwa na kasi ya
wazazi/walezi kupeleka watoto shuleni na kusema ni ndogo
Sweda
amefanya ukaguzi huo shule ya Sekondari Iwawa, Ilumaki, Lupalilo na Mang’oto ambapo
ameagiza kuanzia Jumatano ya wiki hii kutaanza msako mkali kwa Mzazi/Mlezi
ambaye atakutwa hajampeleka mtoto shuleni ili akamatwe na kufikishwa Mahakamani
kujibu mashtaka
Wakati
huohuo mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku walimu kuwarudisha wanafunzi
nyumbani kwa sababu mbalimbali akiahidi kumshughulikia yeyote atakayebainika
kufanya hivyo kwa mwanafunzi yeyote.
Kwa upande wa shule ya Sekondari Iwawa, Kaimu Mkuu wa shule hiyo Mwl. Jitahidi Sanga amesema mapokezi kwa wanafunzi yamekuwa mazuri na anatarajia kufikia Jumatano Januari 12, 2023 wanafunzi wote watakuwa wameripoti shuleni.
Baadhi ya Wazazi waliozungumza nasi ambao ni Suzana Sanga kutoka Ilumaki Sekondari na Mendrad Mwinuka kutoka Mang’oto Sekondari wameeleza kufurahia kupeleka watoto wao Sekondari huku wakiwasihi wazazi wenzao ambao bado hawajapeleka wanafunzi shuleni kuhakikisha wanafuata utaratibu na miongozo ya Elimu ili kukwepa mkondo wa sheria.
Siku
chache zilizopita Mkuu huyo wa Wilaya ya Makete Juma Sweda aliagiza kukamatwa
kwa mzazi yeyote ambaye atabainika kumtorosha mwanafunzi ili kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria au aingie mzazi huyo Darasani kusoma kwa niaba ya mwanafunzi.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO HAPA