MTU anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 jinsia ya kiume anayetajwa kuwa ni mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe.
Tukio hilo ambalo limeonekana kuwashangaza wengi, bado halijafahamika chanzo kikuu ingawa baadhi ya watu wanadai huenda ni matatizo ya akili.
Katibu wa kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtu huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.
"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye vyombo vya usalama ili wajue namna ya kumsaidia,"amesema.
John Kisogo ambaye ni mwinjilisti katika kanisa hilo amesema awali baada ya kumkuta mtu huyo katika madhabahu walilazimika kumfanyia maombi.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO HAPA CHINI