10 watiwa mbaroni sakata la mbolea 'feki' Njombe

 
Jeshi polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 10 kwa madai ya kuhusika na sakata la kuchakata na kuuza mbolea bandia kwa wakulima.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema hayo baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ikiendelea kupekua nyumba ya mfanyabiashara anayedaiwa kuwa muhusika mkuu wa mbolea hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuhakiklisha watuhumiwa wote wanaohusika na sakata hilo la kuchakata na kuuza mbolea bandia kwa wakulima wanachukuliwa hatua.

Pia amewataka wakulima mkoani humo kuwa makini na mbolea wanazonunua na endapo wakibaini kuwa ni bandia watoe taarifa kwa maafisa kilimo wa kata zao.

Tayari Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA) imemfutia leseni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa ndiye mmiliki wa mbolea hiyo bandia.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo