Zungu: Kwanini ufanye ngono wakati huna mke wala mume?

Ikiwa leo Disemba 1, 2022 ni siku ya maadhimisho ya Ukimwi duniani, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu, amelitaka Bunge la vijana 2022 kuwaasa vijana wenzao juu ya kujiepusha na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa kuwa ni kundi linaloongoza kwa maambukizi mapya.


Akizungumza Leo Bungeni Jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa Bunge la Vijana 2022 Mhe. Zungu amesema vijana wafuate maadili kwani hata vitabu vya dini vimekataza suala la uzinifu ndio maana Kwa sasa kundi Hilo la vijana linaongoza kwa maambukizi mpya ya virusi vya Ukimwi

"Na kwanini ufanye ngono wakati huna mke wala mume Biblia imekataza uzinifu na Quran imekataza uzinifu fuateni maadili,hii ndio iwe sehemu la azimio la Bunge hili muwaase vijana ambao wanajiingiza katika matatizo makubwa kwenye umri mdogo"amesema Mhe Mussa Azan Zungu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo