Katika Matokeo ya Darasa la Saba yaliyotangazwa Leo Disemba 1, 2022 na Baraza la Mitihani Tanzania NECTA, Mtahiniwa Iptisam Suleiman Slim wa Shule ya Msingi Chalinze Modern Islamic 'Pre and Primary School' aliyekumbwa na Kadhia ya Kubadilishiwa namba ya Mtihani amefaulu kwa wastani wa Daraja A katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6, 2022.
Katila matokeo hayo Iptisam (PS1408009-0039) Somo la Kiswahili amepata A, English A, Maarifa A, Hisabati B, Sayansi A, Uraia B, wastani wa Daraja A