Jionee Makubwa yaliyoibuka leo Matokeo ya Mtihani Darasa la Saba 2022



Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limezuia matokeo ya watahiniwa 540 kutoka vituo sita vya mitihani ndani ya jiji la Dar es Salaam baada ya kugundulika kufanya udanganyifu


Wanafunzi hao wanatoka katika vituo vya Joylanda, Castle hill, Green Acress, Maktaba, Great Vision na Mtendeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya baraza hilo, matokeo ya watahiniwa hao yanazuiwa hadi uchunguzi juu ya tuhuma hizo utakapokamilika.

“Wakibainika kufanya udanganyifu matokeo yao yatafutwa kwa mujibu wa kifungu Na. 4(8) cha Kanuni za Mitihani 2016 na endapo hawatabainika kufanya udanganyifu watapewa matokeo yao.

Wakati huo pia baraza linazuia matokeo ya watahiniwa 179 ambao waliugua au walipata matatizo na kushindwa kufanya mitihani kwa masomo yote au baadhi ya masomo.

“Watahiniwa hudika watapewa fursa nyingine ya kurudia kufanya mtihani wa Kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2023 kwa mujibu wa kifungu 32(1) cha Kanuni za Mitihani,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo