Kwa mujibu wa Muhudumu wa Chumba cha Kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo, Joseph Mbuthia Githundi, amesema alipigwa na butwaa baada ya kuwaona watu wasiojulikana wakivamia mahali hapo majira ya usiku Desemba 7, 2022.
Amesema, watu hao walichukua maiti iliyotoweka kwenye friji ya mvulana wa miaka 10, na baadaye Polisi kufanikisha kuupata mwili huo ukiwa kwenye tenki lililopo karibu na mochwari na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendela.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa huenda wafanyakazi waliokuwa wakiandamana kupinga kufutwa kazi na Serikali ya kaunti ya Nyandarua walihusika na tukio hilo huku Naibu kiongozi wa Bunge la Nyandarua, Mwangi Kagwe akisema Hospitali hiyo haitapokea miili ya marehemu hadi usalama utakapoimarishwa.