Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya darasa la saba ya mwaka huu likisema watahiniwa zaidi ya 1.07 milioni kati ya 1.34 milioni wenye matokeo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi ametangaza matokeo hayo leo Alhamisi Desemba Mosi, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini hapa kuhusu mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 5 na 6 mwaka huu.