Taarifa Mpya Kuhusu Edward Lowassa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais Samia kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, anayepatiwa matibabu nchini Afrika Kusini. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Rais Samia na kwamba anafuatilia hali ya Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.



Akiwa hospitalini hapo Majaliwa amezungumza na familia ya Lowasa na kuwaambia Rais Samia yupo pamoja na familia hiyo na wanamuombea uponyaji mstaafu huyo.

"Rais anafuatilia kwa kila hatua kuhusu hali ya mheshimiwa Lowasa na anamuombea uponyaji wa haraka," inanukuliwa sehemu ya taarifa hiyo.

Mama Regina, mke wa Lowasa ametoa pongezi kwa Serikali na Rais kwa namna ambavyo wamekuwa karibu na familia hiyo katika kumuuguza kiongozi huyo wa zamani.

Amemuomba Majaliwa kufikisha shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuomba Watanzania waendelee kumuombea Lowasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtoto mkubwa wa Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli, Fredrick Lowasa amewashukuru Watanzania kwamba wamekuwa wakimuombea Mzee wao uponyaji lakini akaomba waendelee hivyo.

Lowasa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete na alihudumu kwa miaka miwili na nusu kabla ya kujihuzulu mwaka 2008 kutokana na kashfa ya Richmond.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo