Mtaka: Hatutaki wanufaika wa TASAF wa kujitakia

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka
Antony Mtaka, Mkuu wa mkoa wa Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka amewataka wazazi kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kujiunga kidato cha kwanza au darasa la kwanza wanawasili shuleni kwa kile alichokieleza kuwa hataki kuendelea kuzalisha wanufaika wa Mpango wa Kusaidia Kaya Maskini (Tasaf) baadaye.


Amesema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga madarasa na kuweka madawati ili wanafunzi waweze kupata elimu hivyo kiasi kidogo cha fedha hakiwezi kukosekana kwa ajili ya kusaidia watu wasiokuwa na uwezo.

Ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 28, 2022 katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa wa barabara mkoani Njombe utakaogharimu Sh108 bilioni.

Mtaka amesema hategemei kuwapo kwa wanafunzi wanaoacha shule na ili kuhakikisha hilo atafanya msako siku ya kufungua shule akishirikiana na watendaji wake.

"Niwaombe wazazi tusije kukwazana kwa jambo hili dogo, Serikali imetoa fedha ya kujenga madarasa, kuweka madawati, hatuhitaji kuzalisha wanufaika wa TASAF huko tunakoenda,"

"Mtu anaacha shule leo tunaleana kwa sababu ya utoro shuleni kesho anazeeka anahitaji serikali impe matibabu ya bure, msaada wa TASAF,"

Amesema ikiwa mtu atakataa shule leo akubali kusajiliwa ili atakapokuwa mzee aadhibiwe kwa kukataa elimu wakati Serikali ilipogharamia kila kitu.

"Tumuambie kuwa kweli wewe ni mzee, unahitaji kuonewa huruma lakini ulikataa shule katikati ya elimu bila malipo, umejengewa darasa, umeletewa walimu na dawati lipo.

"Niwaombe sana wazazi tuhakikishe kuwa watoto wanapaswa kuwa shule Januari 9, na wanapoanza darasa la kwanza wafike darasa la saba na wakianza kidato cha kwanza wamalize kidato cha nne.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo