Ruvu Shootinga Yatangaza Kocha mpya

Klabu ya Ruvu Shooting imemtangaza Mbwana Makata kuwa Kocha wake Mkuu mpya kwa kandarasi ya mwaka mmoja kuziba nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa aliyejiuzulu hivi karibuni baada ya timu kuwa matokeo yasiyoridhisha.


Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema Kocha Makata ni Kocha mwenye historia nzuri katika klabu alizofundisha ikiwemo Dodoma Jiji na Mbeya Kwanza hivyo wanaimani atawapata matokeo mazuri .

"Tulikuwa na kocha wetu Charles Mkwasa na kwa hakika kazi yake tuliifurahia na kuipenda sana na hakuna Mtanzania asiyejua kazi ya yake katika kufundisha mpira.


"Mkwasa ameandika barua kwa uongozi ya kuuomba kuachia ngazi kutokana na mwenendo na matokeo ya timu hasa katika mechi 10 za mwisho za mzunguko wa kwanza ambazo tumeambulia pointi mojatu jambo ambalo halijawahi kutokea," amesema Masau na kuongeza;


Kwa upande mwingine, Bwire amesema Uongozi wa Ruvu Shooting upo kwenye hatua za mwisho za ukarabati wa uwanja wao wa Nyumbani wa Mabatini ulipo Mlandizi mkoani Pwani ambapo ulifungiwa wa Bodi ya Ligi Kuu kwakutokidhi vigezo.


Kikosi cha Ruvu Shooting kinashika nafasi ya pili kutoka mwisho kikiwa na alama zake 11 na tayari kashacheza michezo 15.  


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo