Simba SC yaanika wazi hatma ya Enock Inonga

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amekanusha taarifa za Beki wao kutoka DR Congo Enock Inonga Baka kuwa mbioni kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo aliyesajiliwa Simba SC akitokea DC Motemapembe ya nchini kwao DR Congo, mkataba wake utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Ahmed Ally amesema ni mapema mno kwa sasa kulizungumza suala la Beki huyo, lakini ukweli ni kwamba Uongozi unatambua kuwa Mkataba wake utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Amesema Simba SC imejiwekea utaratibu wake wa kufanya mambo kiofisi, hivyo ni vigumu kwa yoyote kufahamu kinachoendelea ndani kwa sasa baina ya pande hizo mbili.

Hata hivyo Ahmed amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuzipuuza taarifa za Beki Inonga kuwa mbioni kuondoka mwishoni mwa msimu huu, na badala yake waweke imani kwa Viongozi wao, ambao wanafahamu nini wanachokifanya ili kuhakikisha kikosi chao kinakuwa bora.

Simba inafanya kazi zake kwa utaratibu, hatuwezi kuweka kila kitu wazi, suala la mkataba wa mchezaji kuwa katika mazungumzo ama kuondoka linapaswa kuwa kiofisi, kwa hiyo yanayozungumzwa huko nje ni ya kawaida sana.”

“Tunafahamu Inonga ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa kwenye kikosi chetu, ndio maana nimesisitiza kuwa Uongozi unajua nini unachokifanya kwa sasa, Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuwaamini Viongozi na kuachana na maneno ya huko vijiweni.” amesema Ahmed Ally


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo