Wanandoa wawili Tumaini John (41) aliyekuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo Maruku katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba na mume wake Geofrey John (42) mfanyabiashara, wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongana na basi la kampuni ya Happy Nation, lililokuwa likitokea Dar-es-Salaam kuelekea Bukoba.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera William Mwampaghale amesema kuwa ajali hiyo ilitokea Novemba 06, 2022 saa 5:30 asubuhi katika barabara itokayo Bukoba kwenda Biharamulo eneo la Ijuganyondo.
Amesema basi hilo aina ya Youtong liligongana na pikipiki hiyo aina ya SANLG na kusababisha vifo vya watu hao.