Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) iliyoko Gatundu Kaskazini inachunguza kisa ambapo polisi mmoja alilaghaiwa KSh 86,191.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyoonekana na TUKO.co.ke na kunakiliwa kwenye OB nambari 13/8/12/2022, Sajenti Evelyn Karimi Njeru alituma KSh 86,191, mara tatu kwa jamaa aliyetambulika kama Inspekta Peter Mwove.
Ripoti hiyo ilisema kwamba aliyepokea pesa hzio alimuambia Njeru kwamba yeye ni msaidizi wa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (AIG)Jacinta Muthoni huko Vigilance House. Tapeli huyo alimuambia mlalamishi kwamba alikuwa na uwezo wa kumpa uhamisho hadi Benki Kuu ya Kenya kutoka mahala aliko kwa sasa hivi.
"Mtu aliyepokea pesa hizo alijidai kwamba yeye ni msaidizi wa madam Jacinta Muthoni AIG ambaye yuko Vigilance House na alikuwa na ushawishi wa kumpa uhamisho hadi Central Bank of Kenya," sehemu ya ripoti hiyo ilisoma.
Chanzo:Tuko