Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Msisha halmashauri ya wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Joyce Exavery (13) ameuawa kwa kukatwa mapanga akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Ruhita kata ya Kamuli.
Tukio hilo limetokea jana mchana Jumapili Desemba 25,2022 ambapo inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo alifanyiwa ukatili (kuchinjwa) na mtu/watu ambao bado hawajafahamika.
Kamanda wa Polisi wa Kagera William Mwampagale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akizungumza na Malunde 1 blog.
Chanzo: Malunde Blog