Makete
Naibu waziri wa maji ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Makete Mh.Dr.Binilith Mahenge, ametoa msaada wa vitabu zaidi ya elfu moja kwa shule za sekondari zilizopo wilayani Makete.
Katika ziara yake ya siku moja wilayani hapo, Dr Mahenge ametoa vitabu 100 kwa shule ya sekondari ya Mbalatse na vingine 100 kwa shule ya sekondari Lupila ikiwa ni mkakati wake wa kukuza kiwango cha elimu wilayani Makete.
Dr Mahenge pia amefanya Mikutano ya hadhara katika Vijiji vya Mbalatse na Ukange huku akiwataka wananchi Kutambua fursa ya kutumia shule za sekondari za kata na si kutorosha watoto kwenda mjini kufanya vibarua.
Hata hivyo Naibu waziri Dr Mahenge ametembelea Hospitali ya Consolata Ikonda ambapo alielezwa changamoto zinazoikabili hospitali hiyo kuwa ni pamoja na Nishati ya umeme, Ambapo kwasasa wanatumia Jenereta kiasi cha kukwamisha baadhi ya shughuli ikiwa ni pamoja na kitengo cha mifupa.
Akijibu baadhi ya changamoto Mh naibu waziri Dr Mahenge, amesema Baadhi ya changamoto zimeshidwa kutekelezeka kutokana na Ufinyu wa bajeti ya serikali
Na Aldo Sanga