Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema Mkoa huo upo tayari kupokea Watoto 20,235 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023 baada ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa mapya 98 kwa 100% vilivyogharimu Tsh. 1,960,000,000.
Mtaka amesema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya madarasa Njombe yaliyojengwa kwa fedha zilizoidhinishwa na Rais Dkt. Samia “Njombe tumekamilisha ujenzi wa madarasa kwa asilimia 100”
"Nitumie nafasi hii kuwaomba Wazazi wote kila mwenye Mtoto aliyechaguliwa kuja kidato cha kwanza, tarehe 9 January awe hapa, hakuna ada hakuna mchango, hata kama huna uniform njoo shule, kama kuna Mtoto hana uniform asibaki nyumbani kwamba Mimi sina uniform aje kusoma"
Mtaka ameagiza kwamba kama kuna Mzazi yeyote ambaye anajijiua amepeleka Mtoto Mwanafunzi kufanya kazi za ndani amrejeshe kabla ya tarehe tisa ili kuepukana na sheria zitakazochukuliwa dhidi yao.