Baba Mkwe afumaniwa na Mkwe wa Mwanaye

Wanakijiji wa Bumula, Bungoma, wangali na mshtuko baada ya baba mkwe kujiaibisha kwa kuingia kisiri katika chumba cha kulala cha mwanawe wa kiume na kupakua asali ya binti mkwe. 



Mzee huyo mwenye umri wa miaka 65, anayeitwa Masika, ambaye ni mjane, alichukua fursa ya ya kumnyemelea bintiye kwa jina Nafula kwani mwanawe anafanya kazi ya mbali. 


Ikizingatiwa kuwa mwanawe anafanya kazi na anaishi Nairobi, mzee huyo alijenga tabia ya kula chakula cha jioni nyumbani kwa mwanawe kwa kisingizio cha kujumuika na mjukuu wake wa miaka mitatu wakitazama runinga. 


Buda anasemekana alianza kwa kusifia mapishi ya binti huyo ila wakati mmoja alivuka mipaka alipomtania kuhusu jinsi alivyokuwa na figa tamu. Baadaye aliigeuza kuwa mazoea, na wawili hao wakaanza kuvuna matunda haramu.


Mumewe demu huyo alianza kushuku kuwa mke wake ana uhusiano wa kimapenzi kwingine baada ya kuanza kumfanyia mambo ya kihuni. Alibuni visingizio vya kumnyima haki yake ya ndoa alipofika nyumbani, lakini hakujua kuwa ni baba yake mzazi anayekuwa akirina asali. 


Jamaa hata hivyo hakukata tamaa kwani aliamua kufanya uchunguzi wa kina na hata kusaka huduma za mganga maarufu ndiposa ilipobainika kwamba babake mzazi alikuwa akimnyemelea mkewe. Siku chache baadaye, wanakijiji wa Bumula waliamshwa na mayowe kutoka kwa nyumba ya Masika katikati ya usiku. 


Majirani walizunguka boma hilo wakidhani ni wezi lakini walipoingia katika nyumba hiyo wakamkuta Masika akiwa amejibanza kwenye kitanda cha mwanae na mkwewe. 


Haraka walimjulisha mwanawe Simiyu ambaye, kwa bahati, alikuwa Webuye akirejea nyumbani kutoka Nairobi. Kufikia wakati huo, chifu wa eneo hilo na baraza la wazee walikuwa tayari wamefika nyumbani kwa Simiyu, na walikaa kwa subira wakimngojea afike bomani. Simiyu alifika saa moja na nusu baadaye. Baraza la wazee lilijitolea kufanya upatanishi katika suala hilo.


Katika kujitetea, mzee huyo alisema shetani alimshawishi kulala na binti-mkwe wake. Aliomba msamaha na kusihi ahurumiwe, akiahidi kurekebisha njia zake. Mzee alilipa shilingi elfu tano, kondoo wawili kwa ajili ya kujitakasa na jogoo wawili kama adhabu kwa tabia hiyo chwara, ingawa mwanamke alifukuzwa. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo