Mama mzazi mbaroni kwa kumnyonga mtoto wake wa kumzaa

Jeshi la polisi Mkoani Mtwara linamshikilia mwanamke mkazi wa Kijiji cha Sinde  Kata ya  Msangamkuu, halmashauri ya Mtwara,  kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu


Baadhi ya majirani wanasema mama huyo alimnyonga mtoto wake huku yeye na mtoto wakiwa utupu (bila nguo) na kukimbilia porini ndipo majirani walipomkimbiza na kumchukua mtoto lakini alikuwa tayari amefariki


Kaimu Kamanda jeshi  la polisi  Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo