Kaburi la aliyezikwa mwaka 2020 lafukuliwa kwa Amri

Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kivukoni (Kinondoni) jijini Dar es Salaam imeamuru mwili wa mwanamke aliyefia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati wilayani Kinondoni, jijini Dar es  Salaam, mwaka 2020, Stella Moses ufukuliwe na ufanyiwe uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.


Mahakama hiyo pia imeamuru matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe katika vyombo husika ili kama kuna watu waliohusika na kifo hicho wachukuliwe hatua za kisheria.


Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, kufuatia maombi yaliyofunguliwa na wanafamilia wa marehemu. 

Chanzo: Mwananchi Digital


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo