Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuyafumbia macho matukio
ya ukatili yanayojitokeza katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo kwa kuwa
zipo sheria zinazosimamia masuala hayo ili zifuatwe na haki itendeke
Hayo yamebainika leo Desemba 5, 2022 katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa
kisheria tukio lililofanyika kiwilaya katika kijiji cha Kisinga kata ya
Lupalilo wilayani hapo kabla ya kufikia kilele chake Desemba 12, 2022
Akizungumza kwenye ufunguzi huo, Mkurugenzi wa shirika la wasaidizi wa
Kisheria wilaya ya Makete (MAPAO) Mch. Denis Sinene amesema ni wakati sasa wa
jamii ya Makete kuacha kukaa kimya na badala yake waripoti pale wanapoona
vitendo vya ukatili vinapofanyika ili hatua ziweze kuchukuliwa
Amesema watu wanafanya matukio sio kwamba hayapo Makete, matukio yapo lakini watu wanaficha uovu hivyo kijiji cha Kisinga kinatakiwa kubadilika na kuwa mfano wa vijiji vingine vyote vya wilaya ya Makete
Kwa upande wake Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Makete Apollo
Laizer ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maandimisho hayo
amesema matukio yote ya ukatili yanayotokea katika jamii yaripotiwe kwenye
vyombo husika ikiwemo kwa jeshi la polisi kwa kuwa ukatili unapofanyika
hautakiwi kufichwa ndani ya jamii kwa madai ya kusuluhishwa
Amesema vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika katika jamii
ni vitendo vya jinai hivyo sio vitendo vya kusema watu wanakaa mezani na
kuyamaliza hivyo vinatakiwa kupelekwa katika vyombo husika ikiwemo kuvitolea
taarifa polisi katika dawati la jinsia na ikibidi vipelekwe mahakamani ili
mwisho wa siku kuwe na jamii inayozingatia utawala wa kisheria
Aloyce Msigwa, Lucida Salum na Mwl. Zuhura Mussa ni wakazi wa kijiji cha Kisinga ambapo wameieleza Edmo Blog kuwa elimu ya masuala ya usaidizi wa kisheria ifike kwenye kila kijiji kwa kuwa kumekuwa na vitendo vya ukatili vinavyotokea lakini haviripotiwi na vinafanywa kuwa siri, hivyo kushauri vinapojitokeza ni vema vikaripotiwa ili haki itendeke.