Aoa mke wa pili baada ya mkewe kukataa kumfulia nguo

Mwanamke mke wa mtu ameiambia mahakama huko Ndola, Zambia, kwamba mumewe wa miaka 22 alimzunguka na kuoa mke wa pili katika mkoa mwingine.


Katika hadithi iliyochangiwa na Mwebantu, Karen Chungu alifungua kesi ya talaka dhidi ya mumewe Andrew Kapembwa kwa kuoa mwanamke mwingine.


Mwanamke huyo aliyekosewa aliambia mahakama ya eneo la Kabushi kwamba hataki kuwa katika ndoa ya wake wengi ndiyo maana alikuwa akitafuta talaka. Karen alifichua kuwa kuna siku alitarajia kufanya mapenzi na kugundua kuwa Andrew alikuwa amenyoa.


“Nilitaka tuitishe mkutano kwa nini sehemu zake za siri ziko safi, lakini aliniambia ninyamaze kuhusu hilo,” alilalamika. Mlalamishi aliongeza kuwa matatizo katika ndoa yao yaliendelea hadi akamfukuza nyumbani, na wazee walipoingilia alikimbia. Karen pia alifunguka kuhusu changamoto za kushiriki mahaba, akifichua kuwa wawili hao hawakuwa wamefanya mapenzi kwa mwaka mmoja uliopita.


Alipoulizwa maoni yake, Andrew aliambia mahakama kwamba amejaribu kukaa chini na mkewe ili kutatua tofauti zao lakini ilishindikana. "Sikuwa na nia ya kuoa mwanamke mwingine, lakini mke wangu aliacha kunifulia na kutekeleza majukumu yake. Nilioa mwanamke mwingine kwa sababu ya tabia ya mke wangu,” alisema. Andrew pia alieleza kwamba hakuwa akishiriki penzi na Karen kwa sababu sikuzote alikataa mashauri yake. Hakimu Mwandamizi John Kabwe na Hakimu Mwandamizi Emelda Masuwa waliidhinisha talaka hiyo kwa madai kuwa juhudi za maridhiano zilishindikana.


Ingawa Andrew aliiambia mahakama kwamba hataki kuachana na mke wake, ombi lake lilifutiliwa mbali kwa sababu tayari alikuwa ameoa mwanamke mwingine.


Aliagizwa kufidia mkewe K30,000 kwa malipo ya kila mwezi ya K500. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo