Kauli ya Askofu Shoo Matumizi ya Pombe Kali Yaibua Gumzo


KARIPIO la ulevi kupindukia lililotolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, limeibua mjadala huku wanasaikolojia na madaktari wakieleza sababu za kukithiri kwa unywaji pombe na madhara yake.


Katika mahubiri yake kwenye ibada ya Krismasi juzi, Askofu Shoo ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, alikemea kunywa pombe kali kunakofanywa na vijana wa umri mdogo, akionya kuwa wanaharibu afya zao wakiwa na umri mdogo.

Baadhi ya wadau wa afya na saikolojia, wameiambia Nipashe kuwa vijana wenye umri mdogo kuanza unywaji pombe kali, kutawakwamisha kufanikiwa, wakiyataja mabadiliko ya soko huria, uchumi wenye ushindani na ushawishi kuwa sababu ya kundi hilo kujiingiza kwenye ulevi.

Vilevile, wamesema baadhi ya maudhui ya nyimbo nyingi za wasanii yanahamasisha ulevi, hali inayowafanya vijana kupenda kunywa kwa kuwa ni jambo linalohalalishwa.

Akizungumza na Nipashe jana, Daktari Bingwa Mwandamizi wa Afya na Magonjwa ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Saidi Kuganda alisema pombe kali zimo kwenye orodha ya kundi la dawa ambazo zinaathiri akili mara tu zitumiwapo.
Chanzo: Nipashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo