Awaomba Msamaha Wanaume aliowakataa baada ya kuona anazeekea Nyumbani Bila Kuolewa

Mwanamke wa Kitanzania ametangaza hamu yake ya kuolewa hadharani ikiwa hilo litamsaidia kupata mchumba wake wa ndoa haraka iwezekanavyo.


Aliomboleza muda aliopoteza alipokuwa mdogo na akatamani angekubali kuposwa na mmoja wa majamaa waliokuwa wakimjia na pendekezo la kumuoa.


Mwanamke huyo ambaye hivi karibuni anafikisha umri wa miaka 37 alisema ana wasiwasi kadiri muda unavyosonga, lakini wanaume hawaonekani wa kumuoa. Aliyasema hayo yote alipokuwa akiishi nyumbani kwa familia yake akisubiri na kutumaini kwamba wanaume watakuja kubisha hodi wakitaka mdoa naye lakini Ole wake!


Mwanamke huyo alifichua kwamba ameamua kuchukua hatua za kukata tamaa kwani hakuna kitu kinachoonekana kufanikiwa maishani mwake. Alikuwa ametundika mabango njiani kwamba familia yao ilikuwa ikiuza barafu. Kwa njia hiyo, ikiwa mwanamume yeyote angekuja kutafuta bidhaa hiyo, atakuwa kama zawadi kwao.


Aliwaonya wasichana wanaotamani kuolewa siku moja wasikatae mapendekezo ya ndoa wakiwa wachanga. Aliongeza kuwa mwanamke anapokuwa tayari kuolewa, anapaswa kufunga pingu za maisha, kwani akiwa amekomaa sana, hakuna anayeonekana kupendezwa naye. 


Ingawa wanawake wengine wanatamani sana kuolewa, size 8 aliwaonya warembo ambao wanatazamia ndoa kuepukena akuolewa na wanaume ambao hawampendi Mungu. Mhubiri huyo aliendelea zaidi kueleza kuwa mwanamume asiyempenda Mungu hataweza kumfurahisha mwanamke kwani ndoa si kitu rahisi.


Alisema mwanamume anahitaji kumpenda Mungu na mwanamke wake sana na kuwa na mwelekeo. Ni hapo tu ndipo ndoa inaweza kufanikiwa. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo