Jokate Mwegelo aonesha sura ya mwanawe, atangaza jina lake

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ambaye kwa wakati mmoja aliwahi chumbiana na msanii Diamond Platnumz hatimaye amefichua sura ya mtoto wake mchanga na kutangaza jina lake.


Mwegelo ambaye alijifungua wiki chache zilizopita alipakia picha akiwa amempakata mtoto wake mchanga mikononi huku akiwa amejawa na furaha tele.


Alitangaza kuwa mtoto wake huyo jina lake litakuwa ni Totoo na kuwataka watu kwanzia sasa kukoma kumuita Jokate bali mama Totoo.


“Jina lake ni Totoo. Niite mama Totoo, Shukurani zote ni kwa Mungu,” Mwegelo alisema kwa mbwembwe.


Mwegelo ambaye anakubalika sana na Watanzania wengi kwa utendakazi wake aliwahi kuhudumu kama DC kwenye wilaya ya Kisarawe kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Temeke anakokipiga mpaka sasa.


Jokate ambaye alikuwa ni mfanyibiashara na mtangazaji, aliteuliwa na hayati rais Magufuli kama mkuu wa wilaya ya Kisarawe mnamo mwaka 2018 ambapo amekuwa mchapakazi wa kupigiwa mfano si tu Tanzania bali duniani kote kwani mwaka 2017 alitajwa kwenye orodha ya Forbes kuwa miongoni mwa wanawake 30 bora wenye chini ya miaka 30.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo