Mume na mkewe wako rumande baada ya mwanamume kudaiwa kuwapachika mimba mabinti zake wawili katika kaunti ndogo ya Kandara, Kaunti ya Murang’a nchini Kenya.
Mume huyo anasemekana kufanya vitendo hivyo vya kutisha huku mkewe akifahamu kikamilifu matendo yake nyumbani kwao Gichengo-Muruka.
Kulingana na ripoti, mkewe alinaswa baada ya mmoja wa binti zake wanne kukiri kuwa alipachikwa mimba na babake huku mama yake akijua.
Wakazi walisema kwamba msichana huyo wa miaka 14 ambaye alikuwa amemaliza darasa lake la nane alikuwa amepachikwa mimba pamoja na dadake.
Walisema baba huyo alijaribu mara kwa mara kulala na binti zake wote wanne katika matukio tofauti na wengine wawili waliokolewa tu na majirani baada ya kupiga mayowe.