Jamaa mwenye wake wawili akamatwa na kutahiriwa kwa nguvu, Mkewe asimamia zoezi

Mwanaume mwenye umri wa miaka 44, katika kaunti ya Bungoma, alilazimishwa kukabiliana na kisu cha ngariba mbele ya mkewe na watoto wake watatu baada ya kukwepa kisu hicho kwa miaka kadhaa.


Peter Onyango, mkazi wa Lukhome katika kaunti ndogo ya Kiminini alipelekwa mtoni Jumamosi, Disemba 10 asubuhi, na umati wenye ghadhabu, ambapo alipakwa matope kabla ya kuanikwa mbele ya watu kupashwa tohara.


Mkewe, Janet Musenya, alisema kwa muda wa miaka minane tangu walipoana, mumewe alikuwa akikwepa kisu cha ngariba na hivyo kumlazimu kupanga njama ya kutahirishwa kwake.


“Niligundua kuwa anaogopa maumivu lakini sikuweza kustahimili kuishi naye. Nina furaha kuwa sasa ni mwanamume kamili,” alisema.


Aliahidi kutekeleza majukumu yote ya kumuuguza mumewe hadi atakapopona kidonda cha kupashwa tohara. Kulingana na jirani wa wanandoa hao, Amos Sikuku alisema kuwa wanandoa hao walikuwa wanagombana na kwa hasira, mkewe Onyango aliropokwa na kuanika siri yao ya muda mrefu. Lakini Onyango alionekana kuwa na ahueni baada ya kukatwa, akisema alikuwa amekejeliwa kwa miaka mingi kwa sababu ya hali yake.


“Ninawaomba wasamaria wema kusaidia familia yangu kwa chakula katika wakati huuu ambao bado nitakuwa nikiuguza jeraha hili kwani siwezi kufanya kazi yoyote ya maana,” akasema baba huyo wa watoto watatu.


Katika tukio sawia na hilo, wenyeji wa mji wa Chwele katika kaunti ya Bungoma wamejionea kioja cha bure, wakati jamaa mmoja mwenye wake wawili alipokamatwa na umati kisha kulazimishwa kukabiliana na kisu cha ngariba.


Inasemekana kuwa ugomvi wa kinyumbani kati ya jamaa huyo na mkewe wa kwanza ndio chanzo cha mwanamke huyo kumripoti mumewe kwa wazee wa jamii ya wabukusu kuwa hajatairiwa, akiifanya njia mojawepo ya kumtia adabu.

Chanzo: TUKO.co.ke 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo