Milioni 917 Kumaliza tatizo la Maji Ujuni na Nkenja

Mradi mkubwa wa Maji utakaogharimu Milioni 917 unatarajiwa kujengwa katika Kata ya Kitulo Wilaya ya Makete ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji kwa wananchi wa Kijiji cha Ujuni na Nkenja.


Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Antony Sanga mwishoni mwa wiki jana akiwa kwenye ziara ya kuutembelea miradi na vyanzo mbalimbali vya Maji Wilayani Makete Mkoani Njombe.


Akiwa Kata ya Kitulo kukagua chanjo cha Maji ndani ya Shamba la Mifugo Kitulo Mhandisi Sanga amesema ujenzi wa Mradi huo wa Milioni 917 utasaidia kupunguza uhaba wa Maji kwa kuwa kuna maji ya kutosha kwenye chanzo hicho na yataweza kuwanufaisha wananchi kwa kipindi chote cha mwaka bila changamoto.

Mhandisi Sanga pamoja na kuwapongeza wananchi wa Ujuni na Nkenja kwa ujenzi wa nyumba bora za kisasa amewasihi kuendelea kutunza na kulinda vyanzo vya maji kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo hivyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesema Kata ya Kitulo mbali na kuwa na idadi kubwa ya ongezeko la watu pia kuna mradi mkubwa wa Kituo cha Afya ambacho kinahitaji maji kwa haraka kulingana na umuhimu wa huduma zinazotolewa Kituoni hapo

“Chanzo hiki kinauwezo wa kuzalisha maji lita 33.3 kwa sekunde ambazo ni sawa na mita za ujazo 3,000 kwa siku, mradi huu unamihndombinu ya Kilomita 10.4 kutoka kwenye chanjo mpaka kwenye tanki la kwanza, pia tutajenga Tanki la Lita laki moja Kijiji cha Ujuni”.

Diwani wa Kata ya Kitulo amesema uwepo wa ongezeko kubwa la dadi ya wananchi katika Kata ya Kitulo inapelekea changamoto ya maji kuzidi kuwa kubwa na kumuomba Katibu Mkuu Wizara ya Maji kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo