Mwanamke ambaye alikuwa amejaliwa baraka ya mtoto alijikuta akipepea mitandaoni baada ya familia yake na mpenzi wake kumpa bonge la surprise.
Kisura huyo aliposwa na mpenzi wake muda mfupi baada yake kuondoka hospitalini akiwa na malaika wao mchanga.
Mamake mrembo huyo ambaye alishiriki video ya tukio hilo murua kwenye TikTok alisimulia kwamba binti yake alikuwa amejifungua pacha mnamo Julai 21, 2022.
Cha kusikitisha ni kwamba mmoja wa pacha hao, msichana,akiaga dunia. Alisema pacha mwingine, mvulana anayeitwa A’sir, alifanikiwa na hatimaye hospitali iliwaruhusu kuondoka mnamo Desemba.
Binti yake na mpenzi wake walipoondoka hospitalini, familia iliwaonesha pendo kwa kuwasherehekea. Walikusanyika nje, jambo ambalo liliwaacha wapenzi hao wakiwa na hisia na machozi swala lililomlazimu mwanamume moja kuwajongea na kuwaombea mama huyo mpya na mchumba wake. Kisha alianza kutoa hotuba fupi ya kuwashukuru jamaa hao. Baada ya kumaliza mpenzi wake naye aliamua kusema jambo na katika hali ile akampa posa.
Bwana harusi alikaa kwenye kiti cha magurudumu huku bibi harusi akionekana maridadi katika gauni jeupe la harusi walipokuwa wakila kiapo cha ndoa kwenye hafla iliyohudhuriwa na wageni wachache. Picha na video ya kupendeza kutoka kwa hafla hiyo ilizua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakishangilia mapenzi yao.