lori lenye namba T 410 AFR likiwa limeharibika sehemu yenye kona kitu
kinachofanya magari makubwa yasiweze kabisa kupita eneo la Ilamba wilaya
ya kilolo mkoani Iringa
- Na Denis mlowe - aliyekuwa Kilolo
- Magari
yote ya abiria yanayofanya safari zake za kwenda kati ya Iringa mjini
na Kidabaga wilaya ya Kilolo yamekwama kwa wiki baada ya loli lilobeba
magogo kuziba njia maeneo ya Ilamba na kufanya kutokuwa na mawasiliano
kati ya kidabaga na Iringa mjini.
Tukio hilo limetokea wiki sasa kwa mujibu wa madereva wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Iringa mjini na Bomalang'ombe na kufanya magari madogo kupita kwa tabu eneo liliharibika lori hilo lenye namba T 410 AFR kwa upande cabin yake na tela lenye namba T 471 ATY mwenye mali hajajulikana na kusababisha msafara wa mbunge wa viti maalum kuchukua nusu saa kuweza kuvuka eneo hilo kutokana na ubovu wa nafasi lilipoharibika.
Baadhi ya abiria na mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mtandao huu eneo la tukio wamedai kuwa lori hilo lilianza kuziba njia kila linapoharibika kitu kinachofanya magari makubwa yasifanye biashara ya kusafirisha abiria kutokana na ufinyu wa barabara hiyo.

