DC: Hakuna Mpango wa Kumuua Mrisho Gambo


Mkuu wa Wilaya Arusha (DC), Said Mtanda amesema hakuna mpango wowote wa kiongozi wa Serikali kumuuwa Mbunge wa Arusha Mjini (DC), Mrisho Gambo.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne, Desemba 13, 2022, DC Mtanda amesema Serikali haina nia ovu dhidi ya Gambo.

"Nimekuwa nikiona na kufuatilia kwenye mitandao ya kijamii na nimeona ‘clip’ mbalimbali za mbunge Gambo na lengo la kuwaita wanahabari sio kutaka kufanya malumbano na mtu yoyote isipokuwa kutaka kutoa ufafanuzi yale ambayo yanazagaa kwenye vyombo vya habari ikiwepo mitandao ya kijamii," amesema

Amesema alichokisema Gambo kutaka kuuawa, kimewafanya wananchi wamepata sintofahanu kuhusiana na kauli hizo na ni muhimu waweze kufahamu na kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.

"Nina amini mambo mengi yaliyokuwa yakizungumzwa hayana nasaba na kipindi hiki,” amesema mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Arusha na kuongeza:

"Hatufikirii hatujawahi kufikia na Serikali katika wilaya hatuna jukumu hilo, jukumu kubwa la Serikali ni kulinda usalama wa watu na mali zao kumlida mbunge na wapigakura wake," amesema

Mtanda ameshangazwa na taarifa za mbunge huyo kudai anataka kuuawa lakini hajatoa taarifa polisi kwani taarifa ya mwisho aliyotoa kituo cha polisi Muriet ni kuibiwa.

Mkuu huyo wa wilaya amesema, kutokuwa na taarifa za mbunge huyo kutaka kuuawa huku akisema kwa kuwa ofisini zao zipo sehemu moja anaweza kwenda kumpa maelezo. Mtanda amesema anashangaa Gambo kutompa taarifa hizo licha ya kuwa nae kwenye vikao vya CCM jijini Dodoma wiki iliyopita. Wiki iliyopita katika mkutano wake wa hadhara jimboni mwake, Gambo aliibua tuhuma za majaribio mawili ya kutaka kuuawa kwake na watu aliodai ni wa Serikali pamoja na CCM aliodai anawafahamu. Gambo aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema, watu hao wamekwenda kwa nyakati tofauti nyumbani kwake lakini hawakumkuta. Amesema pointi ya kwanza anasema amevamiwa mara mbili lakini waliombamvamia anawafahamu wengine ni watu wa Serikali. Mtanda amesema Gambo pia alizungumza alivyotaka kupewa sumu katika jaribio ambalo lilishindikana. "La mwisho anasema labda njia pekee ambayo watu waserikali wanaweza kufanikisha mpango wao ni labda akiwa anatoka nje ya geti lake kupigwa risasi," 

Mtanda amesema kwanza hali ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Arusha ni shwari lakini pia hata vitendo vile vilivyokuwa vikizungumzwa miaka ya nyuma vya kuondoka usalama na amani Arusha havipo Amesema hakuna mtu wa Serikali au serikali yenyewe ndani ya Jiji la Arusha ambayo Ina Nia ovu dhidi ya Mbunge Gambo. Hata hivyo Gambo Leo alipotakiwa kuelezea ni kwanini hajatipoti polisi tuhuma hizo na kama tayari kuna uchunguzi hakuwa tayari kujibu licha ya kusoma ujumbe wa simu.
Chanzo: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo