Mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga ametangaza vita na vijana wenye umri kuanzia Miaka 14 wasiokuwa na kazi waliokaidi agizo la serikali kulima mazao ya chakula na biashara vijijini katika msimu wa kilimo 2022/23 ambao wamekimbilia mjini kwa lengo la kuzurura na kusema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kiswaga ametanga kuanza kwa msako wa kuwabaini vijana wasiokuwa na kazi rasmi wanaozurura mjini ili kudhibiti wimbi la uhalifu na watakaobaini kujihusisha na uhalifu wakamatwa katika mkutano mkuu wa 27 wa chama kikuu cha ushirika Kahama (KACU).