Bunge la nchini Kenya limegeuka soko la mawindo kwa kina dada ambao wameamua ni lazima wawe kazi kwa kipindi cha miaka mitano pia.
Licha ya kutoshiriki uchaguzi uliopita ili kupewa wajibu wa kuwa waheshimiwa, baada ya vipusa wameamua ni lazima wao pia waonje pesa za bunge.
Kwa mujibu wa gazeti la Nation Jumapili, walinda lango katika bunge wamekuwa na kibarua kila uchao kutokana na warembo wanaofika kuwatafuta wabunge. Duru ziliarifu gazeti hilo kwamba kuna msukumano katika lango kila siku huku vipusa waliovalai kwa namna ya kuanika mapaja nje wakijaa hapo.
"Tunashindwa namna ya kuwakabili kwa sababu hujui kwa ukamilifu wanajuana vipi na mheshimiwa," alisema mlinzi mmoja kwa gazeti hilo. Huku wakihofia kuwakasirisha waheshimiwa, walinzi wamelazimika kutafuta mbinu za kuwakaribisha vipusa hao. Gazeti hilo lilisema warembo sasa wamekuwa wakiwekwa kwenye chumba kimoja karibu na lango kusubiri mheshimiwa wanayemtaka.
Kina dada wa umri mdogo wamekuwa wakimezea mate waheshimiwa na mara nyingi hujipata wamekuwa kitoweo chao. Pesa na magari ya kifahari sawa na ziara za hapa na pale zimekuwa ndio chambo kwa vipusa hawa waliobarikiwa na urembo lakini wakakosa maadili.