Zahanati na Ofisi ya Kijiji zakosa Vyoo, Wananchi wachachamaa

Wananchi wa kijiji cha Ilindiwe kata ya Mang'oto wilayani Makete mkoani Njombe wameeleza kutofurahishwa na usimamizi usioridhisha shughuli za maendeleo katika kijiji chao hali iliyopelekea kutosomewa mapato na matumizi kwa zaidi ya mwaka mmoja pamoja kutolewa kusudio la kufungwa kwa zahanati na ofisi ya kijiji kutokana na kukosa vyoo.


Hayo yameelezwa na wananchi wa kijiji cha Ilindiwe katika mkutano wa hadhara wa dharura ulioitishwa na Diwani kwa lengo la kusikiliza kero ambapo awali ikasomwa barua na Kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Mang'oto Barick Richard kuhusu suala hilo ambapo imeeleza ilani hiyo ilitolewa kwa siku 14 kuanzia Oktoba 15 hadi Novemba 28, 2022 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Lainel Sanga ametolea ufafanuzi suala hilo na kusema kuwa mpaka sasa wapo katika hatua nzuri ya ujenzi wa vyoo hivyo kauli ambayo imepingwa na wananchi wake.
Tazama video hii kwa undani zaidi



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo