Wananchi wa kijiji Cha Ilindiwe wilayani Makete mkoani Njombe wamemueleza diwani wao kwamba hawaridhishwi na kitendo cha Mwenyekiti wa Kijiji hicho Laines Sanga kuendesha kesi za watuhumiwa mbalimbali kwenye ofisi ya kitongoji badala ya ofisi ya kijiji waliyoijenga
Pia wananchi hao wamedai kuwa wengine wanakamatwa usiku na kupelekwa ofisi ya kitongoji jambo ambalo Diwani wa kata hiyo Osmund Idawa amelitolea ufafanuzi kwa kuwaambia kwamba kisheria mwenyekiti anaruhusiwa kufanya kazi kwenye ofisi ya kitongoji lakini isiwe mazoea lakini pia aangalie ni jambo gani anatakiwa kulishughulikia usiku akitolea mfano mauaji au wizi
Tazama video hii Mwanzo mwisho