Watakaokabiliwa na njaa kupelekwa mahakamani


Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Filbarto Sanga, amesema kuwa mkulima yeyote atakayebainika kukabiliwa na njaa atapelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata maagizo ya kuhifadhi chakula waliyopewa wakati wa msimu wa mavuno.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 uliofanyika Kata ya Usevya Halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe, DC Sanga amesema tahadhari imetolewa mapema kabisa mwanzo wa msimu lakini baadhi ya wakulima wataingiwa na tamaa ya kuuza vyakula vyao vyote bila kuweka akiba ya kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashalah, ameshauri wakulima kupanda mbegu bora wakati wa mvua za kwanza ili mazao yapatikane kwa wingi

Kwa upande wao wakulima wamekiri kupokea maelekezo hayo huku wakisema huwa wanauza mazao kwa sababu ya shida zinazowakumba ikiwemo magonjwa na kusomesha.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo