Hakimu agoma kujitoa kesi ya Zumaridi


Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mwanza imetupilia mbali maombi ya mawakili wa utetezi katika kesi namba 12 ya kufanya mkusanyiko usio halali inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake 83 kwa kudai sababu zilizoelezwa hazina mashiko wala sio za kisheria

Mawakili wanaomtetea mfalme Zumaridi waliwasilisha barua mbele ya Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza yenye hoja mbili za kumtaka Hakimu Clescencia Mushi anayeendesha kesi na wenzake kujitoa kusikiliza kesi hiyo

Mawakili hao walieleza kuwa mteja wao analalamikia kutosomewa maelezo ya ushahidi wao mara baada ya kumaliza na pia Hakimu huyo amekuwa anachana karatasi wakati mahakama inaendelea pasipo kutoa taarifa 

Akitoa uamzi huo Hakimu mkazi Clescencia Mushi amesema baada ya mahakama hiyo kupitia hoja zilizoelezwa katika barua iliyowasilishwa na mawakili wa utetezi za kumtaka kujiondoa kusikiliza kesi hiyo, Mahakama imebaini hoja zote mbili hazina mashiko kisheria hivyo ataendelea kusikiliza kesi hiyo

Baada ya kusomwa kwa maamzi ya shauri hilo Hakimu Mushi amesema uamuzi huo hautoi nafasi ya rufaa kwa upande wa utetezi kisheria hivyo akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 15 mwaka huu  ili kuendelea kumsiliza shahidi wa Jamhuri ambaye atamalizia kutoa ushahidi wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo