Kisanga kilishuhudiwa katika mahakama ya Milimani Kenya baada ya wakili kuamua kumlima mume wa mteja wake mahakamani.
Wakili huyo alikerwa na mfanyabiashara ambaye ni mume wa mteja wake katika kesi kuhusu ulezi wa mtoto wao.
Wawili hao walikuwa mbele ya jaji Robert Mbogo katika kesi hiyo wakati wakili Robert Asembo aliamua kumpa mfanyabiashara huyo makonde. Asembo alionekana akirusha kombora la ngumi kabla ya mfanyabiashara huyo kulihepa katika kisa kilichowaacha wanahabari kinywa wazi.Jamaa huyo alionekana mpole huku wakili akitisha kumwangushia makombora zaidi kutokana na kile alisema ni kuita wanahabari kwenye kesi yao.
Mke wa mfanyabiashara huyo amemfikisha mahakamani akisema ametelekeza majukumu yake ya ulezi kwa watoto wao watatu. Mahakama awali ilikuwa imemwagiza mfanyabiashara huyo kulipa karo ya mwanawe aliye kwenye chuo na pia kulipia wawili wengine mahitaji yao.
Ni hali iliyomfanya mkewe kurejea mahakamani tena ili mfanyabiashara huyo ashinikizwe kuchukua hatua hiyo. Katika kisa kingine Embu, ilikuwa ni hali ya kuchanganyikiwa baada ya mkoba wake kuibuka miongoni mwa vitu alizokuwa amedaiwa kuiba mteja wake.
Faith Jappan alikuwa akimwakilisha mteja katika mahakama ya Embu Jumatatu Novemba 7 wakati wa kisa hicho. Alisema alipata kuwa mkosa wake uliokuwa umeibwa awali ulikuwa miongoni vitu ambazo mteja wake alikuwa amedaiwa kuiba.
Chanzo: TUKO.co.ke
