Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Uhifadhi - TAWA wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa Wanne wakisafirisha wanyamapori aina ya Pundamilia watatu na digidigi mmoja wanaodaiwa kuuwawa katika Pori la Karambandeha lililopo kijiji cha Karambandeha wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mbali na watuhumiwa hao pia jeshi la Polisi limekamata pikipiki tatu pamoja na mapanga yanayodaiwa kutumika katika ukataji wa nyama huku likieleza linamsaka mtu mmoja ambaye alifanikiwa kutoroka akiwa na silaha aina ya machine gun inayotajwa kutumika katika kuua wanayama hao.