Mtaka: Siridhishwi na Mgawo wa Maji, Njombe kuna Vyanzo vya Maji Vya Kutosha


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ameongoza Kikao kazi cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi kuhusu mwelekeo mpya wa usimamizi wa huduma ya maji vijijini chini ya Sheria za Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5 ya mwaka 2019.Kikao hicho kilianyika Novemba 04, 2022 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.


Mhe. Antony Mtaka amesema kwamba haridhishwi na kitendo cha mgao wa maji kwani mkoa wa Njombe unavyanzo vya kutosha na idadi ya watumiaji wa maji ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa Bi.Judicar Omari alisema kuwa tunawajibu mkubwa sana wa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

"Mkoa wa Njombe unavyanzo vingi vya maji hivyo tunawajibu wa kuvilinda, mkoa wa Njombe unampango wa kufikia asilimia 85 za upatikanaji wa maji" alisema Bi. Judica.

Akiwasilisha Mada ya sera na sheria ya Maji Mwanasheria wa Mkoa ndugu, George Makacha aliyataja makosa na adhabu anazoweza kupewa mtu kama atavunja sheria kwa kuharibu miundombinu, kuchepusha maji, kutumia maji vibaya, kutupa taka kwenye maji na kuharibu vyanzo vya maji ambapo mtuhumiwa anaweza kupigwa faini ya kuanzia shilingi 500,000/= hadi Milioni 10 au kifungo cha miezi 6 hadi miaka 3.

Meneja wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Vijijini Sadick Chaka alisema kuwa Ruwasa ipo kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na Vyombo vya usimamizi wa huduma za kijamii.

"RUWASA inafanya kazi vijijini hivyo tumejikita zaidi kutoa huduma kwenye maeneo ya vijijini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo