Wafukua kaburi na kunyofoa moyo, ulimi na jicho

Watu wasiojulikana wamefukua mwili wa mwanamke Neema Mlomba mwenye umri wa miaka 26 na kunyofoa baadhi ya viungo vyake ikiwemo moyo katika Kijiji cha Luteba Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amealiagiza Jeshi la Polisi mkoani humo, kufanya uchunguzi wa haraka kuwabaini watu waliohusika na tukio la kufukua mwili wa mwanamke Neema Mlomba na kunyofoa baadhi ya viungo vyake ikiwemo moyo.


Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea Kijiji cha Luteba Halmashauri ya Busokelo ambapo marehemu alifariki akiwa na umri wa miaka 26. 


Homera amesema mbali na moyo viungo vingine vilivyonyofolewa ni Ulimi na jicho la kulia huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.


Mtoto wa marehemu wa Neema yuko hospitali ya Wazazi Meta chini ya uangalizi maalum wa madaktari akiendelea kupatiwa  huduma za matibabu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo