Waandamana hadi kwa Mkuu wa Wilaya kudai kukosa maji

WAKAZI wa eneo la Luguruni Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wameandamana hadi ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James, kwa ajili ya kudai huduma ya maji waliyoikosa kwa miezi mitatu sasa huku wakiletewa ankara(bili).


Wakazi hao wakiwa wamebeba ndoo zao zikiwa tupu walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiashiria kuwa wanahitaji maji huku wanawake wakiziweka kichwani na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo kuwatua ndoo.


Mmoja wa wananchi hayo aliyejulikana kw jina la Emanuel Shirima amesema licha ya mgao wa maji uliopo lakini wao hawajapata maji kwa miezi mitatu sasa lakini bili zimekuwa zikiletwa.


“Mbaya zaidi tunalipishwa bili za maji, pia maji haya tunayoyataka yanapita katika eneo letu, mitaa mingine yanakokwenda wanapata maji ila sisi hatuna.”


“Tumejitahidi kutafuta suluhisho bila mafanikio mwisho tumeamua kuja kwa mkuu wa wilaya atupe suluhu ya suala hili,” amesema Shirima.


Chanzo:Nipashe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo