Video Chafu za wanafunzi zawatokea puani Walimu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea kufuatilia utovu wa nidhamu uliofanywa na baadhi ya wanafunzi wa shule za Wilaya ya Kisarawe wakati wa mahafali ya kidato cha nne.


Amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote walioruhusu vitendo hivyo kufanywa na wanafunzi, akibainisha kuwa uchunguzi wao wa awali umebaini walimu wamewapa wanafunzi uhuru kufanya mambo yasiyokuwa na maadili katika sherehe za shule.


Prof. Mkenda aliyasema hayo jana katika mahafali ya shule za Kiislamu za Ilala yaliyofanyika katika Uwanja wa Garden jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa video hizo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ziliishtua serikali, viongozi wa dini na jamii, wakiwamo wazazi.


"Na ninalaani vikali sana wale walioruhusu ule mchezo wa shule hizo pale Kisarawe na picha zikapigwa, haiwezekani walimu hawakujua, hairuhusiwi na tunaahidi kwamba tutachukua hatua zaidi," alisema.


Waziri Mkenda alisema serikali haitoivumilia shule isiyozingatia maadili mema, akiwaagiza viongozi wa dini kwa kushirikiana na walimu na wamiliki wa shule kuhakikisha suala hilo linakuwa kipaumbele katika malezi ya watoto.


Zaidi<<BOFYA HAPA>>


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo