Jumuiya ya vijana wa chama Cha mapinduzi (Uvccm) wilaya ya Makete, imeupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kuendelea kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana.
Pongezi hizo zimetolewa Kwa niaba ya Jumuiya ya vijana na Katibu wa Hamasa na chipukizi wilaya ya Makete Ndugu Ellymathew Kika katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Pongezi hizo zinakuja ikiwa ni muda mfupi baada ya vijana ishirini kitoka kata za iwawa na Kitulo kupokea mkopo wa pikipiki zenye thamani ya milioni 51.
Kika amesema kutolewa Kwa mkopo huo ambao unatokana na fedha za asilimia kumi ya mapato ya ndani,inawaongezea vijana Hali na Imani na serikali Yao.
amesema mikopo hii kwa vijana inawakwamua kimaisha na kuwajengea uwezo wa kuanzisha miradi Yao ya kibiashara na kujitegemea kiuchumi.
Aidha amesema vijana wengi ambao wamekuwa wakikatishwa tamaa kujiunga kwenye vikundi wanapoona wenzao wanawezeshwa Kwa haraka kupata mikopo hii inawapa Imani kubwa.
Pamoja na pongezi hizo kwa Uongozi wa Halmashauri ya wilaya pia ametoa angalizo kwa viongozi wa ngazi za mitaa na vijiji kuendelea kuwahamasisha vijana kuunda vikundi katika maeneo yao.
Pamoja na hamasa hiyo pia Kika amewaomba viongozi hao kutoa elimu sahihi Kwa vijana ya namna ya uombaji wa mikopo hii ili kupunguza malalamiko ya vijana kuhisi Kuna upendeleo.
Aidha amewaomba waheshimiwa Madiwani pamoja na Mheshimiwa Mbunge kutumia mikutano Yao kuendelea kuwapa elimu vijana kuchangamkia fursa hii na kuwasaidia kuiendesha miradi wanayoombea mikopo.
Katika taarifaa hiyo ya Katibu hamasa na Chipukizi wilaya ya Makete,Kika amesema Uvccm wilaya ya makete Kupitia Mwenyekiti wake,katibu pamoja na viongozi wa Jumuiya wataendelea kufatilia Kwa ukaribu na mahitaji ya vijana na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabiri kwa kushirikiana na viongozi wa serikali.
Pamoja na hayo amewataka vijana kuendelea kuwa na Imani na serikali ya awamu ya Sita chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwani Ina dhamira ya dhati katika kuwasaidia vijana kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira pamoja na kuondokana na umaskini.
