Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai ripoti ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision Air imetoka na kueleza mambo kadhaa ikiwemo Majaliwa kutofungua mlango wa ndege uliopelekea majeruhi kuokolewa
Msemaji huyo mkuu wa serikali amesema kwamba serikali bado haijatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo
"Serikali bado haijatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya kampuni ya Precision air iliyotokea Novemba 6, 2022 huko Bukoba, Taarifa inayosambazwa mitandaoni IPUUZWE kwa kuwa haijatoka katika mamlaka rasmi za serikali, taarifa rasmi itakapokuwa tayari mtajulishwa", - Taarifa ya Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msigwa.