Picha 10 za mabehewa ya SGR yaliyowasili bandarini


Mabehewa yatakayotumika kwa reli ya kisasa (SGR) yameanza kuwasili nchini kutoka Korea Kusini ambapo tayari mabehewa 14 yamepokelewa.

Oktoba 2022 akiwa nchini Korea Kusini, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kiwanda cha Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock inayotengeneza mabehewa ya reli ya kisasa (SGR).


Waziri Mkuu akiwa nchini humo alisema “Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.”


Kipande cha kwanza cha SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kinatarajiwa kuanza kutoa huduma Januari 2023, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameeleza.


Hapa chini ni picha za mabehewa hayo yaliyowasili;









Chanzo: Swahili Times


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo