Mkazi wa kijiji cha Ngulla wilayani Kwimba mkoani Mwanza, Joseph Mathias Mwenye Ulemavu wa ngozi amepoteza maisha baada ya kukatwa mkono wa kulia na watu wanaosadikiwa kuwa na imani za kishirikina, usiku wa manane akiwa nyumbani kwake.
Kutokana na Mauaji hayo, mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, amefika katika kijiji hicho na kutoa siku saba kwa kamati ya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi na kuwakamata wote watakaobainika kuhusika na mauaji hayo.
Kwa upande wake Kaimu Kaimu ACP Mairi Makori amesema mauaji hayo yalitokea usiku wa Novemba 1 mwaka huu na kwamba watu hao walimkata mkono Kisha kuondoka nao.