Kijana anayefahamika kwa jina ya Rahimu Ramadhani (32) mkazi wa kata Sombetini Jijini Arusha, amekatwa mikono yake kwa kisu hadi kuzimia wakati akiwa anafungua mlango wa chumba cha mwanamke ambaye amezaa naye mtoto mmoja Jijini hapa.
Rahimu amesema alifika nyumbani kwa mwanamke huyo aliyezaa naye kwa lengo la kuchukua nguo za mtoto baada ya kufanya mawasiliano naye kwa njia ya simu, lakini alipofika nyumbani hapo aligonga mlango na haukufunguliwa na simu yake iliita bila mafanikio,
Hivyo kulazimika kuingiza mikono akiwa nje ili kuweza kufungua mlango kwa ndani ndipo mwanamke huyo alikata mkono mmoja baada ya mwingine hadi kusababisha kutokwa damu nyingi na mwanaume huyo kuzimia akiwa mlangoni hapo.
Rahimu amesema ameviomba vyombo vya sheria visichukue hatua yeyote kwa mwanamke huyo kwakua duniani anapita tu, na pia endapo akipata nafasi ya kuishi naye hatalipiza kisasi bali atampenda kwa kuwa amesha msamehe.