Rais Samia Suluhu Hassan, amepewa Tuzo ya CARE Impact Award for Global Leadership iliyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Kimataifa la CARE. Tuzo hiyo imetolewa tarehe 10 November 2022, jijini New York Marekani.
Rais amepewa Tuzo hiyo kutokana na Uongozi wake mahiri na wa mfano unaoleta mabadiliko makubwa chanya ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.
Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza, Balozi wa Tanzania nchini Marekani alipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais.