Mbunge Festo: Nauli za Ndege za ATCL zishuke wananchi wengi wapande ndege

Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga amekosoa gharama za bei za safari za ndege za Shirika la Ndege nchini (ATCL) na kuomba serikali iingilie kati ili wananchi wa kawaida waweze kuutumia usafiri huo kwa shughuli za kiuchumi.


“Nchi hii imewahi shuhudia shirika la ndege binafsi la Fast Jet likirusha Air Bus kwa safari za Dar es Salaam na Mwanza na maeneo mengine kwa bei ya chini ambayo watanzania wengi walifurahia kusafiri na usafiri wa ndege”.

Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Mapango wa Taifa.

Sanga amesema: "Ukikata tiketi ya DSM kwenda Katavi ni sawa na kukata tiketi ya kwenda nje ya nchi, bei hizi zinakatisha tamaa kwa Watanzania kutumia usafiri wa ndege kwenye kuharakisha shughuli zao za kiuchumi. 

"Sasa hizi za Air Tanzania ni ndege zetu Watanzania, viwanja ni vyetu kwanini bei zipo juu sana? Naomba serikali ilitazame hili kwa maslahi mapana ya nchi yetu". amesema Sanga


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo